The House of Favourite Newspapers

Dully Sykes: Nitaonyesha mke sio mchumba

HITMAKER wa Ngoma ya Kadamshi ambaye pia ni mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amesema kamwe hawezi kumuonyesha mwanamke ambaye hajamuoa kwenye jamii kwa sababu ameshajifunza mengi sana kupitia wasanii wenzake waliothubutu kuonesha wanawake walio nao kwenye uhusiano.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Dully alisema kuwa kwanza kabisa hana mwanamke kwa sasa lakini kama akimpata atafaidi sana kwani mambo ya kidunia mengi kayaacha kwa sababu hakuna ambalo hajalifanya.

 

“Hakuna kitu kibaya kama unatoka na mwanamke unaachana naye anaenda kutembea na rafiki yako ni kitu kibaya mno na cha fedhea sana, hivyo nitamuweka wazi mke wangu, sio msichana tu ambaye wakati wowote unaweza kuachana naye,” alisema Dully.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.