The House of Favourite Newspapers

Duma: Bongo Movi Inatia Kinyaa

Daudi Michael ‘Duma’

Na ALLY KATALAMBULA| GAZETI LA AMANI| SHOW BIZ XTRA

MSANII wa filamu aliyewahi kutamba na tamthiliya ya Siri ya Mtungi ‘Duma’ amesema kwa sasa hali ya sanaa ya maigizo nchini inatia kinyaa kutokana na baadhi ya wadau wa filamu kutotambua misingi ya fani hiyo. Akipiga stori na Amani,

Daudi Michael ‘Duma’

Duma amesema: “Ukiitizama kwa kina  fani hii ya sanaa ya maigizo kwa hapa Bongo kwa sasa inatia kinyaa, baadhi ya wasanii wanaochipukia hususan wa kike wamekuwa na tabia ya kutoa rushwa ya ngono kwa waandaaji wa sinema ilimradi wapewe sini za kucheza kwenye filamu husika.

Wasanii ambao wamekuwa tayari kutoa miili yao kwa thamani ya kupewa nafasi ya kucheza kwenye filamu husika ndiyo ambao wakishapata majina wamekuwa hawaishiwi skendo za ajabu kila kukicha. Bongo Muvi haina heshima tena, imepoteza thamani, watu wasio na sifa wamevamia fani hii, kwa sasa kila mtu anatuona wote tulio kwenye fani hii ni wahuni,” alisema Duma.

Comments are closed.