The House of Favourite Newspapers

DUMA: Mimi ni Bosi, Gabo Muigizaji!

MSANII wa filamu Bongo, Daudi Michael ‘Duma’ amefunguka juu ya tetesi zinaendelea mitandaoni kwamba yupo kwenye bifu zito na msanii mwenzake Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ hazina ukweli.

Akipiga stori na Amani, Duma alisema hayupo katika bifu na Gabo kama watu wa mitandao wanavyovumisha ingawa hana mawasiliano naye kwa sababu hana kitu cha kuongea naye ila akiwa na kazi anaweza kufanya naye na akamlipa.

“Sina bifu naye kabisa na wala hatuna mawasiliano kwa sababu mimi ni bosi wa kampuni yeye ni msanii wa kuigiza sasa tutaongea kuhusu nini? Labda nikiwa na kazi nitamwita afanye na nitamlipa ila najua yeye hawezi kuniita kwa sababu hajawahi kuzalisha filamu,” alisema Duma.

Stori: Shamuma Awadhi, Amani

Comments are closed.