The House of Favourite Newspapers

‘Dume Suruali’ ya Mwana FA na ‘Muziki’ ya Darassa ni Habari Nyingine Kabisa Huko Youtube

MWANAFA-NEWVideo ya ‘Dume Suruali’ ya mkali wa Rap, Mwana FA aliyomshirikisha Vanessa Mdee pamoja na video ya ‘Muziki’ ya Darassa aliyomshirikisha mkali wa RnB, Ben Pol ndizo video za muziki wa rap Tanzania zinazoongoza kwa kuangaliwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa muda mfupi hivi sasa tangu ziwekwe wiki takribani mbili zilizopita.
Video hizo zimeonekana kuchuana vilivyo kwa mashabiki wao kuziangalia mara nyingi zaidi zikigusa rekodi ya kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya kipindi kisichozidi wiki mbili tangu zilipopandishwa mtandaoni.
darassa-4
Muziki ya Darassa imeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 1.44 tangu ilipopandishwa kwenye mtandao huo Novemba 23 mwaka huu huku ‘Dume Suruali’ ikiangaliwa zaidi ya mara milioni 1.13 tangu ilipowekwa YouTube Novemba 25 mwaka huu.
Hii inaonesha kuwa hivi sasa wasanii wanaungwa mkono zaidi na mashabiki wao kwa kuangalia video zao kwenye mtandao kutokana na uwepo wa mapinduzi ya kiteknlojia, ambapo mamilioni ya Watanzania sasa wanaweza kupata ‘internet’ kwenye simu zao.
 Darassa ft Ben Pol – Muziki ( Official Music Video )

MwanaFA Featuring Vanessa Mdee – Dume Suruali (Official Music Video)

Comments are closed.