The House of Favourite Newspapers

DYANAMIC AMFUNGUKIA BARAKA THE PRINCE

0
dyanamic amfungukia baraka
Barakah The Prince

MSANII wa Bongo Fleva anayebamba na Ngoma ya Kamoyo, Hamadi Abdulhemed ‘Dynamic’ kwa mara ya kwanza (dyanamic amfungukia baraka),  amemfungukia msanii mwenzake, Baraka Andrew ‘Barakah The Prince’ kuwa ndiye aliyempa jina la Dynamic.

 

Akichonga na Over Ze Weekend, Dynamic alisema tangu aingie kwenye muziki huo, Barakah amekuwa akimpa msaada mkubwa katika muziki na hata shoo anazofanya.

 

“Nimeshapanda na Barakah kwenye shoo kubwa mbili, sijui kwa wengine labda wanaoona anajisikia kwangu hayupo hivyo. Ni mtu poa sana na nimekuwa nikishirikiana naye mara kwa mara kwenye muziki,” alisema Dynamic anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Kosa Langu na Rafiki wa Kweli.

STORI: OVER ZE WEEKEND

Leave A Reply