The House of Favourite Newspapers

Dylan Kerr ampa jukumu Samatta la kuiua Algeria

0

Martha Mboma, Dar es Salaam

BAADA ya mshambuliaji Mtanzania wa TP Mazembe, Mbwana Samatta kuibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika na timu yake kutwaa ubingwa, Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amefunguka kuwa straika huyo anatakiwa kucheza kwa kujiamini kuhakikisha anaibeba Stars dhidi ya Algeria Jumamosi.

Kerr alisema kuwa Samatta ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji na uwezo wa kufanya vizuri zaidi na amefanikiwa kumshuhudia akiitumikia timu ya taifa hapa nchini, hivyo akishirikiana vyema na wenzake, anaweza kuifikisha mbali Stars.

Akizungumza akiwa Afrika Kusini, kocha huyo alisema mshambuliaji huyo anatakiwa kujituma kwa bidii akishirikiana na wenzake ili kuweza kuandika historia nzuri zaidi kwa Waarabu hao.

“Samatta nimeona uwezo wake kupitia mechi za timu ya taifa ya hapa Tanzania lakini ni mmoja ya wenye vipaji ambao nchi hii inatakiwa kujivunia pia kutokana na kufanya vyema akiwa na klabu yake ya TP Mazembe, sasa ni wakati wa kuonyesha kweli anaweza kwa kuiongoza Stars dhidi ya Algeria akishirikiana na wenzake.

“Cha msingi anatakiwa kujiamini na ajitume uwanjani, atafanikiwa na kuweza kufika mbali zaidi ya hapo alipo sasa, hasa kipindi hiki ambacho ana jukumu zito kuisaidia timu yake ya taifa,” alisema Kerr.

Leave A Reply