Dyna Nyange: Tunaumizwa wasanii wa kike tunapodhalilishwa

Dayna-nyange7MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Dyna Nyange hivi karibuni ametoa dukuduku lake la moyoni kuwa anaumizwa na unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa kwa wasanii wa kike na hivyo amewataka watu wanaofanya vitendo hivyo kuacha mara moja kwani bila hivyo litashusha heshima ya wasanii wa kike nchini.

 Akizungumza na mwandishi wetu, staa huyo wa Kibao cha Mafungu ya Nyanya alikwenda mbele zaidi na kusema kwamba hata yeye mwenyewe amekwishawahi kufanyiwa vitendo hivyo tena katika kipindi ambacho aliupata ustaa, ulimyumbisha na kumuumiza hivyo anazijua changamoto zake.

“Huwa inaumiza, wakati mwingine mtu fulani anakwambia huwezi kutoka bila kulala nami kwani wengi waliopita kwake wametoka kwa staili hiyo. Kwa kweli huwa inaumiza, ni changamoto ambayo sisi kama wasanii wa kike tunatakiwa kulivalia njuga suala hili ili wahusika waache mara moja hata kwa kuwataja majina yao hadharani,” alisema Nyange.


Loading...

Toa comment