Ebitoke aapa kumzalia Mlela

YA Mungu mengi! Ukimsikia komediani Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ utacheka, maana mwenyewe ameapa kumzalia mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa kiume wa Bongo Movies, Yusuf Mlela. Ebitoke ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, anawashangaa wanaomponda kwamba haendani na Mlela,

lakini ukweli ni kwamba lazima amzalie ndiyo watafunga midomo. “Mimi ninajiuliza, kwa nini watu wanachonga sana kuhusu uhusiano wetu? Sasa hivi najipanga kumpa Mlela zawadi ya motto ndiyo watu watafunga midomo,” alisema Ebitoke ambaye kapo yake na Mlela ni gumzo Bongo


Loading...

Toa comment