The House of Favourite Newspapers

Ebitoke, Dk Shika Waiteka Dar Live (Pichaz + Video)

Dk Shika akiongea na wananchi katika usiku wa ‘900 Itapendeza’ uliofanyika katika ukumbi wa burudani wa Dar Live Mbagala-Zakhem, jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
…Akitambulishwa kwa mashabiki na mmoja wa waandaaji wa hafla hiyo.
…Akipandishwa kuelekea kwenye steji.
Msanii wa vichekesho nchini, Ebitoke, akifanya yake stejini na baadhi ya wasanii wa kundi lake la Timamu Media usiku wa kuamkia leo.

 STAA wa vichekesho Bongo, Ebitoke pamoja na ‘bilionea’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, Dk Louis Shika usiku wa kuamkia leo, waliuteka Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar baada ya kupokea shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki.

Katika usiku huo uliokwenda kwa jina la Usiku wa Itapendeza, Dk Shika aliongea na wakazi wa jiji la Dar kuwaelezea maisha yake kiurefu jambo lililowasisimua wengi waliojitokeza na wengine kushindwa kuzuia hisia zao na kutoa vitambaa na kujifuta machozi.

Dk Shika aliwaeleza jinsi alivyotoka Tanzania kwenda Urusi na maisha ya huko yalivyokuwa magumu kwake pale alipotekwa na maharamia kisha kufanikiwa kuwatoroka wengi walibubujikwa na machozi alipowaeleza kuwa alipondwa vidole na kung’olewa meno kwa koleo bila kutumia ganzi.

Mbali ya bilionea huyo wa nyumba za Rugumi kueleza maisha yake kilefu pia kulikuwa na burudani za kupendeza kutoka kwa Ebitoke, Jahazi Modern Taarab, African Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii wa kizazi kipya Linex na wengine kibao.

Kwa upande wa Ebitoke aliyepanda jukwaani na kundi lake zima kutoka Timamu, liliwafanya mashabiki wavunjike mbavu kwa vicheko kutokana na mambo ambayo waliyafanya jukwaani akiwa sambamba na mamaa Ashura.

“Hii ni burudani ya aina yake jamani tumeiona hii sikukuu ya Uhuru kuwa tamu kweli kwetu hawa jamaa wa Dar live wametufurahisha sana leo,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hamisi Mkunje.

Stori: Issa Mnally | Global Publishers

Comments are closed.