The House of Favourite Newspapers

Ebitoke: Mlela Atarudi Kwa Magoti

SIKU hizi kuna usemi usemao bana mpaka penati! Ndivyo anavyoonesha mchekeshaji wa kike, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ baada ya kutokubali kama mpenzi wake Yusuph Mlela amemsaliti kwa mwanamke mwingine.

 

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Ebitoke alisema anachojua Mlela atakuja kwa magoti na ndiyo maana mpaka sasa hivi anaogopa kupokea simu yake hata kuwasiliana naye kwa sababu anajua amemkosea.

 

“Kuumia naumia sana lakini nachojua Mlela atakuja kwa magoti muda si mrefu na watu wasirubuniwe na uzuri wa yule demu, maana hawajui nini nampa Mlela, atakuja tu muda si mrefu,” alisema Ebitoke.

Comments are closed.