The House of Favourite Newspapers

Ebitoke: Nimemuahidi Ben Pol Kumpa Kitu Chochote Anachokitaka (Pichaz + Video)

0
Mchekeshaji anayekuja kwa kasi Bongo, Ebitoke (kushoto) akifanya mahojiano na Kelvin Shayo wa Global TV Online siku ya jana Mbezi jijini Dar. Nyuma ni mabaunsa wawili wanaomlinda Ebitroke aliopewa na Ben Pol.
…Akiendelea kufanya mahojiano.
…Akiwa katika pozi na camera man wa Global TV Online, Hilary Daudi (kulia).

…Akieleza hisia zake kwa Ben Pol.
Wakiagana baada ya mahojiano. 

Siku chache baada ya Ben Pol na mchekeshaji anayekuja kwa kasi Bongo, Ebitoke ku-make headlines baada ya kukutana na kupiga picha zinazowaonesha wakiwa kimahaba, ikiwa ni baada ya mwanadada huyo kulalama kwa siku nyingi kwamba anampenda msanii huyo wa Bongo Fleva, Global  TV Online imemtafuta Ebitoke na kufanya naye mahojiano.
Katika mahojiano hayo, Ebitoke alisema kwamba watu wengi wanadhani kwamba ni kiki lakini kiukweli amefurahi sana kukutana na Ben Pol na kupiga naye picha pamoja na kupata nafasi ya kumueleza hisia zake live.
Ebitoke amesema hawezi kueleza nini kitafuatia kati yake na Ben Pol lakini amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa sababu ni kweli anampenda kwa dhati na yuko tayari kumpa chochote.

Leave A Reply