Ebola Yaua Uganda, Shughuli za Zasitishwa, Tanzania Yatoa Tamko

Serikali ya Uganda imewataka raia wake katika mpaka na DR Congo kusitisha shughuli zote za kijamii zikiwamo masoko, sherehe, mazishi na mikusanyiko mingine. Ni baada ya mtoto wa miaka 5 kufariki kwa Ebola wilayani Kasese, na pia mdogo wake na bibi yake kubainika kuwa na Ebola.

 

tayari Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, imeshatoa taarifa kwa wananchi wake kuchukua tahadhari za ugongwa huo.

“Tumepokea kwa tahadhari ya uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda. Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikichukua hatua za utayari (preparedness) za kukabiliana na ugonjwa huu. Wananchi wasiwe na hofu. Tutatoa taarifa kwa umma siku chache zijazo.” Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

 


Loading...

Toa comment