The House of Favourite Newspapers

Ecobank Tanzania Yasherehekea Ukuaji Wake Ulioambatana Na Mafanikio Ya Ecobank Group

Mkurugenzi wa Ecobank Tanzania, Dr. Charles Asiedu akizungumza na vyombo vya habari.

Ecobank Tanzania imetangaza ukuaji na mafanikio yake katika robo ya kwanza ya mwaka 2024, ambayo ni muendelezo kutoka matokeo yao chanya katika mwaka wa fedha 2023, Benki hii imeonyesha kutambua mchango mkubwa na ushirikiano wa wateja, wadau na wafanyakazi wao katika kuleta mafanikio haya.

Katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka, mapato yaliongezeka kwa 66% hadi kufikia karibu TZS 10 bilioni ikilinganishwa na robo ya kwanza ya 2023 kufuatia ongezeko la mikopo kusaidia uchumi wa Tanzania na ongezeko la kasi ya biashara iliyoimarishwa na kukubalika kwa huduma mbalimbali za benki kwa wateja.

Faida kabla ya kodi ilikua karibu mara 5 ikilinganishwa na robo ya kwanza ya 2023, ikifikia TZS 3.5 bilioni, na kuifanya benki kuwa miongoni mwa benki zinazofanya vizuri zaidi sokoni. Ukuaji wa faida uliungwa mkono na punguzo la gharama mbalimbali pamoja na uwiano wa Mikopo isiyolipika (NPL) kuwa chini ya 3% kwa miaka miwili iliyopita.

Ufanisi wa uendeshaji uliendelea kuboreka kutokana na upanuzi wa tofauti kati ya mapato na gharama. Hivyo, uwiano wa gharama kwa mapato ulipungua hadi chini ya 60% kwa mara ya kwanza ikilinganishwa na 77% mwaka mmoja uliopita.

Mkurugenzi wa Ecobank Tanzania, Dr. Charles Asiedu alisema, “Matokeo haya ya kuvutia yanaonyesha kuongezeka kwa imani ya wateja katika biashara yetu kwa maana ziliongezeka kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa 68% hadi TZS 313 bilioni, na hivyo kupelekea ukuaji wa mali kwa 27% hadi TZS 415 bilioni. Kutokana na ukuaji mkubwa wa amana, tuliweza kusaidia biashara za wateja wetu kwani tuliongeza mikopo yetu kwa zaidi ya TZS 65 bilioni hadi TZS 157 bilioni kutoka TZS 90 bilioni.”

Matokeo ya Ecobank Tanzania kwa mwaka 2023 yalikuwa ya kipekee ambapo mapato yaliongezeka kwa 48%, ya kufikia TZS 31.26 bilioni, kutoka TZS 21.11 bilioni mwaka 2022. Faida kabla ya kodi (PBT) iliongezeka sana kwa 496%, kutoka TZS 1.61 bilioni mwaka 2022 hadi TZS 9.59 bilioni mwaka 2023.

Uwiano wa gharama kwa mapato ya benki uliongezeka sana, ukipungua kutoka 90.56% mwaka 2022 hadi 65.1% mwaka 2023, ikionyesha mikakati madhubuti ya usimamizi wa gharama. Kitabu cha mikopo na mapato kilikua kwa 79%, kutoka TZS 91.75 bilioni mwaka 2022 hadi TZS 164.50 bilioni mwaka 2023.  Amana za wateja ziliongezeka kwa 48%, kutoka TZS 185.97 bilioni mwaka 2022 hadi TZS 274.59 bilioni mwaka 2023, zikionyesha mahusiano mazuri na imani ya wateja katika huduma za Ecobank.

Jumla ya mali iliongezeka kwa 27%, ikifikia TZS 406.69 bilioni mwaka 2023.

Kwa ubora wa matokeo haya, benki inashikilia nafasi ya juu katika sekta za kibenki na kuongoza kwa kiasi kikubwa katika vipimo muhimu vya sekta. Ecobank Tanzania inashikilia nafasi ya tatu kutoka juu kwa jumla ya asilimia zake za mali kwa 26.7%. Zaidi ya hapo, ikiwa na 48.33% ya amana za wateja, Ecobank Tanzania imeonekana kuaminika kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha za wateja, huku ikiongoza kwa mikopo na malipo ya awali kwa kiasi cha 79.3%.

Vilevile, asilimia ya mapato ya Ecobank Tanzania ya 48.5% inaakisi uzalishaji wake mzuri wa mapato ikilinganishwa na benki zingine. Takwimu hizi zinadhihirisha utawala na ushindani wa Ecobank Tanzania katika sekta ya benki, na hivyo kuimarisha nafasi yake ya kuwa mdau mkuu katika soko.

Mafanikio haya yanawiana na mafanikio mapana ya Ecobank Group, ambayo ni jumuiya ya huduma za kifedha barani Afrika. Licha ya mazingira yaliyokuwa na changamoto kiuendeshaji mwaka 2023, Ecobank Group ililiripoti faida kwenye usawa wa wanahisa wa 24.9% na kuongeza faida kabla ya kodi kwa 8% (au 34% kwa sarafu ya kawaida) na kufikia Dola za Kimarekani Milioni 581.

Mapato halisi yalivuka alama ya Dola Bilioni 2 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015, yalikua kwa 11% (au 31% kwa sarafu ya kawaida) hadi kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 2.1.
Ecobank Tanzania imejitolea kuimarisha huduma zake, kupanua wigo wake na kukuza ushirikiano utakaochochea ukuaji na maendeleo ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania. Benki itaendelea kujitolea kusaidia wafanyabiashara na watu binafsi kufikia malengo yao ya kifedha, na kuimarisha zaidi nafasi yake kama mdau mkuu katika sekta ya benki nchini Tanzania.