The House of Favourite Newspapers

Efm Redio Kugawa Pesa kwa Wasikilizaji Wake

0
Sehemu ya washiriki wakitafuta vitu vilivyofichwa katika uwanja huo.
Washiriki wa mchezo wa Sakasaka wakisubiri kuhakikiwa vitu walivyoviokota kama ni sahihi.
Mtangazaji wa Efm redio Chogo akimuhoji Neema Mukurasi kuthibitisha kitu kilicho okotwa na Aisha Idrisa (wakwanza kushoto) ambae alijishindia shillingi Milioni moja.
Meneja matukio Efm redio Neema Mukurasi (wakwanza kulia) akiwa ameshikilia vitu vitatu vilivyo okotwa na mshiriki Mr. Denis Charles (wakwanza kushoto ) vyenye thamani ya shilingi Laki mbili wakiwa na Mtangazaji Denis Rupia (Chogo).
Meneja matukio, uhusiano na mawasiliano Neema Mukurasi akimkabidhi mmoja wa washiriki wa mchezo huo shilingi elfu 50 baada ya kuokota kitu chenye thamani hiyo.

Efm redio imezindua rasmi msimu wa tatu wa mchezo wa sakasaka. Mchezo huu huchezeshwa kila mwaka na mwaka huu utachezeshwa katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo, Ilala na Bagamoyo. Siku ya jana tarehe 28/05/2017 ulizinduliwa rasmi katika Uwanja cha Sinza Tippi Wilaya ya Ubungo.

Mchezo huu wa sakasaka huchezeshwa kwa kuficha vitu vyenye thamani ya pesa katika uwanja husika ambapo inampasa msikilizaji afatilie dondoo za kitu hicho pamoja na mahali ili ajue sehemu na aina ya kitu kilichofichwa na atakae kipata atakua mshindi wa pesa taslimu.

Mwaka huu washindi nane katika kila wilaya watajishindia pesa taslimu, ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shillingi milioni moja akifuatiwa na washindi wa shilingi  laki moja na elfu hamsini.

Leave A Reply