Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha redio cha Efm wakifanya usafi katika Hospitali Teule ya Tumbi.…Wakiendelea na kazi hiyo. Wakifanya usafi eneo hilo.Usafi ukiendelea.
Meneja wa Efm, Dennis Ssebo (katikati) akiwa katika mazoezi ya Joggin kabla ya kufanya usafi.
Wafanyakazi wa Efm wakiendelea na Jogging.
Msanii chipukizi wa Singeli akiimba stejini.
Mkurugenzi wa Efm Redio, Francis Ciza akiwavisha medani washindi walioingia tano bora kwenye michuano ya Singeli katika Wilaya ya Kibaha.
KITUO cha redio cha Efm kilichopo Kawe-Mikocheni jijini Dar, chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom jana kilisepa na kijiji katika tamasha lao lijulikano kama Muziki Mnene na kutua katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Pwani ambapo wafanyakazi wa kituo hicho walifanya usafi kama ishara ya kampeni iliyozunduliwa na rais Dk. Magufuli mwaka jana.
Mbali na wafanyakazi hao kufanya usafi eneo hilo pia kituo hicho kilielekea katika Uwanja wa Bwawani, Kibaha, Pwani, na kuendelea na michezo mbalimbali ambapo baadaye kilihami katika baa ya Kontena.
Katika tamasha hilo, burudani ilikuwa ya aina yake na shangwe kila kona kutoka kwa mashabiki waliofurika katika baa hiyo pale walipokuwa wakipanda wasanii wanaokuja kwa kasi kupitia muziki wa Singeli.
Tamasha hilo, lilizinduliwa rasmi Agosti 27, mwaka huu ambapo, Meneja wa Efm, Dennis Ssebo, alisema lengo kubwa ni kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na Mkoa wa Pwani, kwa namna walivyoipokea Efm Radio na kushirikiana nao hadi kufikia sasa.
Alisema tamasha la Muziki Mnene mwaka huu linafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo muziki unapigwa katika baa 12 za Jiji la Dar na Pwani likiwa limebeba kauli mbiu ya ”TUNASEPA NA KIJIJI” ikiwa na maana kuwa, kila wiki Efm inaweka kambi katika kijiji kimoja ama eneo moja kwa muda wa siku nne.
Aidha muziki mnene eneo husika unapokuwa umetua huenda sanjari na kampeni ijulikanayo ‘NJE NDANI’ ambapo vipindi vinne vinarushwa moja kwa moja (live) katika mtaa husika ambavyo ni Uhondo (Siku ya Jumatano), Sports Headquarters (Alhamisi), Joto la Asubuhi (Ijumaa) na Funga Mtaa (Jumamosi) na burudani kutoka kwa RDJ’s Mamy wa Efm.
Pia kwa muda wa asubuhi, Muziki Mnene unapokuwa umetua panakuwa na Jogging, muziki wa Singeli, michano kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki ambapo anayeibuka mshindi hupewa fursa ya kupigiwa nyimbo zake kupitia radio hiyo na mpira wa miguu kati ya timu ya Efm na timu za Maveterans wa eneo husika.
Na Hilaly Daud/Gpl
Comments are closed.