The House of Favourite Newspapers

EFTA, GSM Kuwakomboa Wanyabiashara Wadogo na Kati

Taasisi ya kifedha ya EFTA na GSM  zimesaini mkataba wa makubaliano ya kusaidia wafanyabiashara wadogo na kati kukuza biashara zao kupitia mikopo nafuu isiyo na dhamana  ya vifaa, magari na vitendea kazi ili kujiimarisha kiuchumi ambapo ni muendelezo taasisi hiyo katika kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi nchini, kuwawezesha vifaa kama mashine na magari.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Makampuni ya  GSM,  Benson Mahenya amesema wameamua kushirikiana na EFTA  kutokana na kutambua  umuhimu wa shughuli  za uzalishaji wanazozifanya pamoja na wateja wao.

Mkurugenzi wa makampuni ya GSM Group ,Benson Mahenya akibadilishana nyaraka na mkuu wa Masoko na mauzo wa kampuni ya EFTA nchini Clerius Asiel baada ya kusaini makubaliano ya kuwakopesha vitendea kazi ,Magari na mitambo wafanyabiashara wanaouza bidhaa za kampuni ya GSM bila dhamana jijini Dar es salaam .Katikati ni Mkurugenzi wa viwanda na uzalishaji Yassir Nassor.

Mahenya amesema kupitia mkataba huo, mawakala na wadau wanaosambaza bidhaa zao ambao wanakosa mikopo kwa vigezo vya kawaida wataweza kupata mikopo ya magari kutoka EFTA kupitia dhamana yao.

“Naamini kwa kufanya hivi tutagusa maisha ya kila mtu na kuongeza thamani ya biashara wa wadau wetu na kuongeza msaada,”

Ameeleza kuwa kutokana na shughuli nyingi wanazofanya ikiwemo usalishaji wa vinywaji,  pia wamejikita zaidi katika kuimarisha usafirishaji wa matunda kama malighafi ili kuondoa uharibifu.

” Sisi tumeona ni vyema tukaimarisha usafirishaji wa matunda kwa kwenda eneo la uzalishaji ili yasiharibike na kupotea pia kumpa thamani mkulima,” amesema.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mauzo na Masoko wa EFTA Tanzania, Clerius Asiel amesema  kwa zaidi ya miaka 20 wamekuwa nguzo muhimu kwa wafanyabiasha wadogo na kati nchini kwa kuwasidia kuwasaidia kumiliki mashine na magari kwa mikopo nafuu bila dhamana.

Ameeleza kuwa mkataba huo na GSM umekuja baada ya kuwezesha upatikanaji wa magari zaidi ya 60 ya kusambaza bidhaa za kampuni hyo.

“Hatua hii ni kielelezo cha maono yetu ya pamoja ya kukuza biashara endelevu, huku tukiwa na mchango wa moja kwa moja katika uundaji wa ajira na kuboresha kipato kwa wafanyabiashara wadogo.

“Kwa kuingia makubaliano haya  GSM wanatupa nafasi ya kufanya biashara na  wadau wao wote. Yaani leo hii kama ni mdau  wa GSM ukihitaji kifaa chochote cha kusaidia katika biashara yako, taasisi ya EFTA itakupatia mkopo kuanzia wa  mwaka mmoja hadi miaka mitatu    na hii itawezesha kumiliki magari au mitambo mbalimbali itakayosaidia katika shughuli zao iwe   matrekta kwa dhughuli za kilimo na Maroli kwa shughuli za usafirishaji “, amesema Asiel.

Amefafanua kuwa kwa mwaka jana pekee wameweza kutumia zaidi ya bilioni 48 kwa wakulima, wafanyabiashara na wajasiriamali  pia EFTA imeweza kuwakopesha mashine na mitambo wachimbaji wadogowadogo katika mikoa ya kanda ya ziwa alimaliza  Asiel.