The House of Favourite Newspapers

El Chapo Aomba Msaada kwa Rais Obrador Kurejeshwa Mexico

0
Mlanguzi wa dawa za kulevya Joaquin ‘El Chapo’ Guzman

RAIS wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador amesema atazingatia ombi la mlanguzi wa dawa za kulevya Joaquin ‘El Chapo’ Guzman, anayetumikia kifungo kurejea Mexico kutoka Marekani kumalizia kifungo chake kwa misingi ya kibinadamu.

Mwanzilishi wa genge la ulanguzi la Sinaloa ameomba msaada kwa Rais Obrador, kutokana na madai ya mateso ya kisaikolojia ambayo Guzman, anasema anateseka katika gereza la Marekani.

Rais Obrado aliwaambia wanahabari kwamba wanapitia maombi ya El Chapo. Haikuwa wazi kama Mexico ilikuwa na uwezo wa kukubaliana na ombi hilo.

Mwaka 2019, Mahakama ya serikali kuu mjini Brooklyn nchini Marekani ilimhukumu kifungo cha maisha jela El Chapo baada ya kupatikana na hatia ya kufanya biashara hiyo haramu iliyosababisha vifo vya watu wengi na kuingiza nchini Marekani tani nyingi za dawa ya kulevya.

SAKATA LA SALMA BIRIANI KUPIGWA AKIWA AMEFUNGWA PINGU,KULAZWA KABURINI, KUFANANISHA NA MWIZI

Leave A Reply