The House of Favourite Newspapers

Mwanariadha Kipchoge Aweka Rekodi ya Marathon

MWANARIADHA wa Kenya, Eliud Kipchoge, amekuwa binadamu wa kwanza kukimbia mbio ndefu (marathon) kwa kutumia muda wa saa 1 dakika 59 na sekunde 40 katika mashindano INEOS yaliyofanyika huko Vienna Jumamosi iliyopita.

Amekuwa ni binadamu wa kwanza kukimbia mbio hizo kwa kutumia muda ambao ni chini ya masaa mawili.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 34 ameingia katika  Kitabu cha Rekodi cha Guiness japokuwa ushindi huo hautatambliwa na shirikisho la kimataifa la riadha — IAAF.

 

Comments are closed.