Akaunti ya Trump ilifungiwa kwa muda wa miezi 22 na uongozi uliopita wa Twitter, kwa madai ya kukiuka sheria na kanuni za mtandao huo kwa kuhamasisha vurugu.
Hata hivyo, siku chache zilizopita, Elon aliwataka watumiaji wa Twitter kutoa maoni yao kama Trump arudishiwe akaunti yake au laa ambapo matokeo ya kura asilimia 51.8 waliafiki suala hilo huku asilimia 48.2 wakitaka Trump asirudishwe.
“Watu wameamua. Trump anarudishwa,” aliandika Elon kupitia ukurasa wake wa Twitter kuhusu akaunti ya Trump ambayo ilifungwa baada ya wafuasi wake kulivamia Bunge la Marekani, baada ya matokeo ya uchaguzi kutoka na kuonesha kuwa Joe Bidden ameshinda.