The House of Favourite Newspapers

Elon Musk Ataka Mmiliki wa Twitter Kumtetea Mahakamani

0
Elon Musk na Bosi wa zamani wa Twitter Jack Dorsey

BILIONEA namba moja duniani, Elon Musk amechukua hatua za kisheria kumwita mwanzilishi mwenza wa wa mtandao wa Twitter, Jack Dorsey kufika Mahakamani akiwa kama mtetezi wake kuhusu kusitisha malipo ya zaidi ya Tsh. Trilioni 102 ili kuinunua Twitter.

 

Mawakili wa Musk walimpigia simu bosi wa zamani wa Twitter, Jack Dorsey ambaye anatajwa kuwa na urafiki na Elon wakimtaka kutoa msaada wa utetezi na kukubaliana na mmiliki huyo wa Tesla kuwa Twitter hawasemi ukweli kuhusu watumiaji ghushi wa mtandao huo.

Elon Musk, Bilionea namba moja duniani

Upande wa Twitter nao wanamuomba Jaji anayesikiliza kesi hiyo kumuamuru Elon Musk ambaye ni tajiri wa kwanza duniani kukamilisha ununuzi wa kila hisa kwa bei ya Tsh. 126,394 kama walivyokubaliana awali.

 

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa huko Delaware, nchini Marekani mnamo Oktoba kama manunuzi na muuzaji hawatakuwa wamefikia makubaliano ya kawaida ya kumaliza biashara hiyo.

Leave A Reply