Kartra

Eneo la Kale la Kutengeneza Mvinyo Lagunduliwa Israel

JENGO la miaka 1,500 la kutengeneza kinywaji aina ya divai, ambalo linasemekana kuwa kubwa zaidi duniani wakati huo, limegunduliwa nchini Israel na wanaakiolojia.

 

Mitambo mitano iligunduliwa kwenye duka kubwa la wauzaji wa enzi za Byzantine huko Yavne, Kusini mwa Tel Aviv, ambayo inakadiriwa kuwa ilizalisha lita milioni mbili kwa mwaka.

Baada ya mchakato wa kisasa wa uzalishaji ulisafirishwa karibu na Mediterania. Wale wanaofanya kazi katika eneo hilo walielezea kushangazwa kwao na ukubwa wake. Kuna mpango wa kufanya eneo hilo kuwa kivutio cha wageni baada ya shughuli ya kupahifadhi kukamilika.

Kinywaji hicho kilikua na sifa ya ubora wa ali ya juu katika eneo zima la Mediterranea, lakini wakati huo divai pia ilikuwa chakula kikuu kwa wengi.


Toa comment