Hersi: Si Kibwana Tu, Simba Wanataka Mabeki Wetu Wote na Viungo

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya YANGA, Eng HERSI SAID amesema amepata tetesi za viongozi wa klabu ya Simba hivi karibuni kuonekana mara kadhaa nyumbani kwa wazazi wa beki kinda wa YANGA Kibwana Shomari.

 

“Ninazo taarifa hizo kupitia mchezaji mwenyewe na watu wangu wa karibu kuhusu ziara zenye nia ya kumshawishi beki wetu kijana ili ajiunge nao, Lakini nikwambie tu sisi kama Yanga tupo kisasa mno siku hizi hizo mbinu zao ni za kizamaniĀ  kama wanaume kweli waje mezani walete mzigo, huo ujanja ujanja wao hautawasaidia kamwe.

 

“Siyo Kibwana tu ambaye wanamnyatia tunazo taarifa nyingi kuhusu wachezaji wetu karibia ‘back line’ yetu yote wanaitaka, halafu kiungo chetu chote wanakitaka winga zetu wanazitaka. Sasa sijui wana hela kiasi ganiĀ  na mimi siwashangai hawana ‘scouting’ nzuri ya kutafuta wachezaji.

 

“Timu waliyonayo inaitwa asante AZAM, sababu wachezaji wote waliotamba nao miaka mitatu iliyopita walipewa kama sadaka na Azam, sasa wanawaona wamezeeka na wamechoka wanataka tena kitonga ndiyo ‘choko choko’ unaziona hizo ila kwetu hawawezi wao waingie sokoni watafute wachezaji waunde kikosi chao hayo mengine waachane nayo wala hawawezi kutusumbua vichwa tulishatoka huko,” alisema Eng. Hersi.2180
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment