The House of Favourite Newspapers

Enock Bella Aachia Ngoma Mpya, Adai Hana Baya na Wenzake

0
Enock Bella ameachia ngoma mpya yenye miondoko ya singeli inayofahamika kwa jina la NDOA

MSANII wa Bongo Fleva aliyetamba na kundi la Yamoto Band Enock Bella ametembelea Studio zetu za Global TV na 255globalradio ambapo pamoja na mambo mengi tuliyoongea naye amesema hawezi kuwalaumu wenzake kutompatia sapoti kutokana na kwamba kwa sasa kila mtu ana maisha yake na washakuwa wakubwa.

 

Enock Bella amethibitisha kuwa kwenye album mpya ya Beka Fleva kuna ngoma amefanya naye na ni ngoma kali kiasi kwamba wapenzi wa muziki wataipokea vizuri.

Enock Bella alitamba na kundi la Yamoto Band

Alipogusiwa uhusu kufanya kazi na Mbosso pamoja na Aslay amedai kuwa nyimbo na Mbosso ni suala la muda tu lakini lazima itoke hiyo ni lazima kwahiyo wapenzi wa muziki wasubiri kwa hamu kazi yake na Mbosso kuhusu Aslay amedai Aslay yupo bize sana kuna nyimbo alimtumia lakini kutokana na kubanwa hajafanikiwa kufanya naye kazi.

 

Msanii huyo ambaye ametoa nyimbo yake kwa mara ya kwanza ndani ya studio za Global TV na 255globalradio inayokwenda kwa jina la NDOA yenye miondoko ya singeli.

 

Leave A Reply