The House of Favourite Newspapers

Enock Bella: Awaambia Mashabiki Hatubebwi na Aslay

0

 

Msanii wa Yamoto Band Enock Bella a.k.a The Base.

MMOJA wa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band,  Enock Bella a.k.a The Base,  amesema wamechoshwa na maneno ya mashabiki wao kuwa mwanamuziki mwenzao, Aslay,  anawabeba na ndiyo maana wameanza kufanya kazi kama ‘solo artists’  ili kila mmoja aweze kuonyesha uwezo wake wa kuimba peke yake bila kundi.

Pia amefafanua stori za chini ya kapeti kuwa yeye bado hajapata menejimenti.

“Kwa sasa hakuna mtu ambaye hajapata menejimenti kati yetu wanne,  mimi ninayo menejimenti yangu ila siwezi kuiweka wazi kwa sasa hadi nitakapoachia wimbo wangu mpya ambao upo jikoni.

“Mashabiki wangu wakae mkao wa kula, huenda kukawa na surprise kwenye huo nyimbo kwani naweza nikaja na staili tofauti ya kubana pua,” amesema Enock Bella.

Leave A Reply