Enock Bella: Walionizushia Kifo Wamenipotezea Dili Nyingi

Baada ya hivi karibuni kuzushiwa kifo, hatimaye msanii wa Bongo Fleva, Enock Bella ameibuka na kueleza kuwa waliomzushia jambo hilo wamemsababisha kukosa dili nyingi za kazi zenye fedha nyingi hivyo kuwataka waache na wasijaribu kurudia tena.

 

Akipiga stori na Showbiz, Enock alisema alipata wakati mgumu sana baada ya kuanza kupigiwa simu nyingi na watu wake wa karibu ambao walikuwa wanamwambia kwamba wameona taarifa zake za kufa mtandaoni, jambo ambalo si kweli.

 

“Unajua nilikuwa napokea simu nyingi sana kutoka kwa watu wangu wa karibu, sasa wanashangaa kuona mimi ni mzima kwani baada ya kuona taarifa mtandaoni kwamba nimekufa walishuka sana na kuna shoo mbalimbali nilikuwa nikafanye nje ya nchi lakini zimesitishwa baada ya kusikia nimekufa.

 

“Nilifikia hatua ya kwenda kuwashitaki wote waliohusika kusambaza habari hizo lakini nikaona bora nikae kimya tu niwasamehe maana hawajui walitendalo ila ukweli ni kwamba wameniharibia dili zangu nyingi sana kwa sababu kuna watu ambao walitaka kufanya kazi na mimi sasa baada ya kuona zile taarifa wakasitisha,” alisema.

MEMORISE RICHARD

Toa comment