The House of Favourite Newspapers

Ervixy: Belle 9, Prezzo wananipeleka kimataifa

0

ervixyErvixy

Stori: Boniphace Ngumije

Msanii Mbongo anayefanya shughuli zake za kimuziki nchini Kenya, David Kallanja ‘Ervixy’ amefunguka kuwa kolabo yake ya Wimbo wa Hapo aliyowashirikisha Abedinego Damian ‘Belle 9’ na Jackson Makini ‘Prezzo’ ni ya kimataifa kutokana na heshima waliyonayo wasanii hao.

belle91Belle 9

Ervixy ambaye ni msanii kutoka Lebal ya Sappy Music amesema kichupa cha ngoma hiyo kinachotarajiwa kuanza kuonekana kideoni leo kimefanywa na Prodyuza Hanscana na kutokana na kilivyotulia lazima kitoboe anga za nje.

prezzo (2)Prezzo

“Nashukuru mambo yamekwenda vizuri, Ijumaa (leo) natambulisha kichupa cha ngoma ya Hapo, niko na Belle pamoja na Prezzo, kiukweli nakiona mbali sana maana Hanscana amefanya yake,” alisema Ervixy.

Leave A Reply