ESHA AVUNJA UKIMYA KUACHANA NA MUMEWE

Esha Buheti

DAR ES SALAAM: Baada ya tetesi kuenea kwenye mitandao ya kijamii mwigizaji wa Bongo Muvi, Esha Buheti ametandikwa talaka na mumewe, hatimaye mwanamama huyo amevunja ukimya.  

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa juu ya tetesi hizo, Eshe alisema hata yeye anashangaa watu wanavyosema ameachwa wakati bado wapo pamoja na hawana dalili yoyote ya kuachana ndiyo maana hakuona sababu ya kuwajibu maana watu wa mitandao ameshawazoea.

“Nimeona watu wanaandika sijui mimi nimeachwa na mume wangu na maneno mengi ya uongo hadi nikabaki nimeduwaa, nikaishiwa la kusema wakati bado nipo naye wala hatuna ugomvi ila mitandaoni sijui wameyatoa wapi, nadhani aliyesambaza hizo taarifa alikuwa na hasira tu hakuwa katika hali yake ya kawaida,” alisema Esha.


Loading...

Toa comment