The House of Favourite Newspapers

Esha Buhet: Usanii ushanibumia, bora niuze

0

EsheBuhetiMsanii wa filamu hapa Bongo, Esha Buhet.

Imelda Mtema

MSANII wa filamu hapa Bongo, Esha Buhet amefunguka kuwa kwa upande wa usanii anaona umeshaenda kombo hivyo kuliko kukaa tu bora afanye ujasiriamali wa kushona kofi a za nywele.

Akizungumzia maisha yake ya sasa baada ya soko la filamu kuonekana kutolipa, Eshe alisema kwa hali ya maisha ilivyo ujanja ni kutafuta kazi mbadala ya kufanya na yeye ameamua kufanya biashara hiyo ambayo angalau inamlipa.

“Mimi kwa kweli inawezekana labda usanii niliingia kwa bahati mbaya sana naona ndiyo maana hata mafanikio yake yalikuwa ni matatizo sana, sasa nimeona kuliko kukaa barazani na kupiga soga, bora nishone kofi a za nywele, nipate vijihela ili maisha yaendelee, mjini hapa…ohooo,” alisema Esha.

Leave A Reply