ESMA AANIKA BATA LA MAMA D, MUMEWE DUBAI

Esma Khan

 MWANAMAMA maarufu kwenye mitandao ya kijamii (socialite) ambaye ni dada wa staa wa Afro- Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan ameanika bata walilopewa na kaka yao huyo huko Dubai.  Kufuatia kusambaa kwa picha za mama wa staa huyo, Sanura Kassim ‘Mama D’ na mumewe, Anko Shamte wakila bata kama lote huko Dubai, Esma alisema kuwa siku zote Diamond amekuwa akitaka familia yake iwe ya kwanza katika kila kitu na yeye ndiye chanzo cha bata lote hilo.

Esma aliliambia Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu akiwa Dubai kuwa, bata hilo walilopewa na kaka yake huyo ni sehemu ya kupata muda mzuri na familia yake kwa maana mara nyingi anakuwa na kazi hivyo kukaa pamoja inakuwa ni shida.

“Diamond anapenda sana familia yake kuliko kitu chochote. Hili bata siyo mara ya kwanza, lakini ndiyo anapata muda mzuri wa kukaa na familia yake na pia alisisitiza kufanya hivyo ni kuzidi kuonesha ni jinsi gani yupo karibu na familia yake,” alisema Esma.

Esma aliongeza kuwa kitendo alichofanya Diamond cha kuwapa familia yake bata hilo ni kizuri kwa sababu familia inapofurahi, hasa mama yake mzazi ndivyo anavyozidi kupata baraka. “Diamond anazidi kufanikiwa kwa sababu anajali familia yake hasa mama yake mzazi hivyo baraka zinazidi kuwa nyingi sana kwake,” alisema Esma ambaye naye yuko kwenye bata hilo akiungana na Mama D, Shamte, Rommy Jones na jamaa aliyetajwa kwa jina la Juma Lokole.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Toa comment