Esma Aanika Ukweli Mimba ya Queen Darleen

 

Kumekuwa na tetesi kibao zikidai kuwa huenda ndoa ya Queen Darleen na mumewe Isihack tayari imeshajibu baada ya mrembo huyo kutoka WASAFI kudaiwa kunasa ujauzito.

 

Mara nyingi kila akiulizwa, Darleen amekuwa akilikwepa suala hili na kutotoa majibu sahihi lakini kwa upande wa dada wa mwanamuziki Diamond, Esma Platnumz,   amekuwa akisema mara zote kuwa Darleen ana mimba.

 

Leo Esma amezidi kupigilia msumari suala hilo baada ya ku-comment kwenye video ya Darleen na mumewe kwa kuandika: ”Halafu hii mimba inaanza kukukondesha ujue umepungua kidogo.”

 

Hii inazidi  kuchochea hisia kwamba huenda kweli  Darleen ana mimba.

 

Toa comment