The House of Favourite Newspapers

ESMA ATOBOA SIRI ZA PETIT MAN

 

Image result for esma na petit man

UKITAJIWA jina la Esma Khan unaweza kusitasita kidogo na kudhani huenda nakutajia majina ya waigizaji kutoka India lakini ukweli ni jina la Kibongo kabisa.  Kwa wafuatiliaji wa muziki wa Bongo Fleva na habari za kidaku bila shaka watakuwa wanaijua familia ya staa wa muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na katika familia hiyo yupo Esma Khan ambaye ni dada yake.

Huwezi kumkuta akiigiza, kama kuuza sura ‘video queen’ alishaufanya kipindi hicho kaka yake anatoka kimuziki katika video ya Wimbo wa Kamwambie. Esma ametokea kujipatia umaarufu mkubwa husan kuwa karibu na familia hiyo ambayo hufuatiliwa na mashabiki wengi. Ijumaa limemfungia safari hadi dukani kwake, Sinza-Afrikasana na kufanya naye Exclusive Interview na katika makala haya anatoboa hadi siri za aliyekuwa mumewe ambaye pia ni mzazi mwenzake, Petit Man.

Ijumaa: Hivi Esma mtoto wako huwa hamkumbuki baba yake maana kwa sasa haupo naye nyumbani?

Esma: Anamkumbuka tena sana tu sasa atafanyaje na baba yake ndio kashanogewa na penzi jipya (anacheka).

Ijumaa: Penzi jipya kwani yupo na nani?

Esma: Si huyo mtoto wake Gadner jamani mbona mnajifanya hamjui wakati mnajua kila kitu.

Ijumaa: Kumbe ni kweli wapo katika uhusiano na huyo mtoto wa Gadner (Karen)?

Esma: (kicheko) kama nilivyosema bana msinichote maneno mimi kwani hamjui mbona hata wanaishi pamoja jamani sio siri tena.

Ijumaa: Kwa hiyo mapenzi yapo moto kumbe?

Esma: Ohooo! Kama yote!Image result for esma na petit man

Ijumaa: Kwa hiyo mpango wa kuolewa tena huna au?

Esma: Kwa sasa hapana kwa kweli mpaka nipate mwanaume sahihi sitaki kukurupuka.

Ijumaa: Unataka mwanaume wa aina gani sasa hivi?

Esma: Napenda mtu mzima ambaye kashamaliza ujana halafu ‘Gentleman’ nitulie naye utoto utoto hapana kwa sasa maana kinyago ukichonge mwen-yewe mwisho wa siku kinakutisha mwenyewe sitaki mimi nimejifunza.

Ijumaa: Mbona unasema kinyago umeki-chonga mwenyewe unama-anisha nini?

Esma: Nafikiri nikisema hivyo mwenye uelewa atanielewa.

Ijumaa: Kwa hiyo huna mpango kabisa wa kurudiana na baba mtoto wako.

Esma: Sina kabisa kwa kweli kwa sababu sipendi anayoyafanya na ndio maana nimehama nilipokuwa naishi naye nimepanga kwingine na nina maisha yangu.Image result for esma na petit man

Ijumaa: Kuhusu mwanaume ambaye unamuhitaji uwe naye kwa sasa unaweza ukafunga naye ndoa?

Esma: Ndio, ili mradi awe na sifa ambazo nimezihitaji namaanisha anayejielewa aliyemaliza mambo yote ya kiujana na kujua kuwa anaishi na mimi bila kupeana stress.

Ijumaa: Vipi eti watu huwa wanadai wewe huwa unamtegemea kaka yako (Diamond Platnumz)?

Esma: Nafikiri unaona hapa (kicheko) upo dukani kwangu vitenge kama vyote na vipodozi kwa sasa ni mwendo wa kutafuta hela tu kwa sasa mambo ya mapenzi tupa kule nipo single mpaka apatikane huyo ninaye muhitaji.

Ijumaa: Vipi ‘wananzengo’ wanadai kuwa wewe ni ‘Yuda Eskarioti’ maana ukiona upepo unaenda huku na wewe hukohuko.

Esma: Utawaweza wananzengo kawaida yao kusema mimi nashukuru huwa siwaogopi hata chembe.

Ijumaa: Kwa hiyo unamwambia nini Petit Man?

Esma: Wakati yeye anahangaika na kujirusha na kula raha mimi natafuta hela kwa nguvu zote.

MAKALA: NEEMA ADRIAN NA SHAMUMA AWADHI

Comments are closed.