VIDEO: Esma Platnumz KUIBA Mume Wa Baby J, UKWELI WAANIKWA!!

Mwanamuziki kutoka visiwani Zanzibar, Jamila Abdalah ‘Baby J’ (kushoto) akifanya mahojiano na Mwandishi Mkongwe, Imelda Mtema, kupitia Global TV Online.

HAPATOSHI! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia sakata linalomgusa Esma Khan baada ya kudaiwa kumpora mwanaume aliyejulikana kwa jina la Abood ambaye ni mzazi mwenza wa mwanamuziki kutoka visiwani Zanzibar, Jamila Abdalah ‘Baby J’.

 

Kikizungumza na gazeti hili, chanzo cha uhakika kilidai kuwa, mwanaume huyo ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na Baby J, alianza kwa kuomba ushauri kwa Esma ambaye ni dada wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Ilidaiwa kuwa, jamaa huyo alikuwa akimtumia Esma kwa ushauri baada ya kutokea kwa ugomvi kati yake na mzazi mwenzake ambapo alikuwa akimfuata dukani kwake, Sinza, Afrika-Sana jijini Dar.

“Zamani Baby J na Esma walikuwa wana ukaribu, lakini mzazi mwenza wa Baby J alikwenda dukani kwa Esma kisha kumuelezea mgogoro wake na msanii huyo. Ilielezwa kuwa Esma alimpigia simu Baby J na kuzungumza naye ili kuyaweka mambo sawa. Kikiendelea kuzungumza, chanzo hicho kilitiririka kuwa, baada ya muda mfupi ndipo Esma na jamaa huyo wakaanza kuonesha ukaribu uliotia shaka.

 

Kilisema kuwa, baadaye zilianza kusambaa picha zikimuonesha Esma na Abood wakiwa pamoja kwenye pozi matata. Baada ya kukisikiliza chanzo hicho kwa makini, gazeti hili lilimtafuta mwanaume huyo na kumuuliza kinachoendelea ambapo alijibu kuwa anamheshimu sana Esma na hakuna chochote cha mapenzi kati yao.

 

“Esma wanayemsema ninamchukulia kama ndugu yangu, dada yangu wa karibu na sina uhusiano wowote wa kimapenzi na yeye. “Pia mambo yangu binafsi sipendi kuyaweka wazi hata kidogo,” alisema Abood.

 

Kwa upande wake, Baby J alipoulizwa kuhusu habari hizo za kuporwa mwanaume alisema kuwa yeye anamuachia Mungu kwa sababu hana la kufanya, lakini wakumbuke yeye ana mtoto mdogo na bado alikuwa akihitaji malezi ya baba na mama.

 

“Mimi ninamuachia Mungu kwa sababu Esma siyo kwamba hanijui au sijawahi kuongea naye kama marafiki, lakini kwa yaliyotokea sina la kuzungumza,” alisema Baby J.

 

Gazeti hili lilizidi kwenda mbele zaidi na kuzungumza na Esma kuhusu madai hayo ya kupora mwanaume wa mwenzake ambapo alisema kuwa, huyo Abood hana cheti cha ndoa, wala pete mkononi hivyo amewaomba watu wampumzishe. “Jamani nimeiba mwanaume wa mtu? Wanaosema hivyo hivi huyo mwanaume ana cheti cha ndoa? Au pete kidoleni? Hebu niacheni jamani nipumzike,” alisema Esma ambaye hivi karibuni ndoa yake ya Petit Man ilivunjika.


Loading...

Toa comment