The House of Favourite Newspapers

Esma: Hata Iweje, Sirudiani na Peti

Esma Khan, akiwa na na mzazi mwenziye, Petit Man.

DADA yake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan, amefunguka kuwa, hata iweje, hawezi kurudiana
na mzazi mwenziye, Petit Man.

 

Esma amefunguka hayo kufuatia kuvuja kwa video mtandaoni ikiwaone- sha wawili hao waki- wa pamoja na wadau kuanza kuwapongeza wakidhani wamerudiana.

 

“Hatujarudiana. Hiyo video ni ya siku nyingi, wewe an- galia hata hizo nguo tulizovaa sidhani hata kama wote tunazo hadi sasa, ni za siku nyingi sana. Kwa

sasa mimi jamani hata iweje siwezi kurudiana na Petit,” alisema Esma. Septemba, mwaka huu, Esma alitan- gaza rasmi kumwagana na Petit kwa kile ali- chodai kuwa jamaa huyo amekuwa akimkwami- sha katika mambo yake ya kimaen- deleo.

Stori: Memorise Richard

Comments are closed.