ESMA HATAKI KUSIKIA KUHUSU NDOA TENA

Esma Khan

DADA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan amefunguka hataki kusikia tena kitu kinachoitwa ndoa kwa sababu mara nyingi mtu unaweza kupoteza muda wako kuitengeneza ndoa na kuilinda kumbe mwenzako hana mpango.  

 

Esma aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, kuwa kwa sasa hawezi kukimbilia tena kwenye ndoa kwani katika ndoa yake ya awali hakuna alichokivuna hivyo bora ajikite kwenye kusaka pesa.

 

“Kwa lugha nyepesi, sitaki kusikia wala sihitaji tena ndoa. Hata mtu akija akasema anataka kunioa, nitajua ni walewale tu kwani mapenzi ya dhati siku hizi hakuna,” alisema Esma aliyewahi kuolewa na meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Petit Man kisha ndoa yao kuvunjika.


Loading...

Toa comment