ESMA: NIMEMMISI MOBETO

 

Esma Khan ‘Esma Platnumz’

WIFI zilipendwa! Dada wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond platnumz’, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ amefunguka juu ya urafiki wake na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto na kusema alikuwa rafiki mzuri kwake hivyo anammisi.  Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Esma  alisema kati ya watu ambao huwa akikaa anawamisi, mmojawapo ni Mobeto kwa kuwa alikuwa ni rafiki mzuri kwake ingawa watu wengi hawalijui hilo.

“Sijasema hivi kwa kutafuta kiki jamani ila nimeongea ukweli kutoka moyoni. Misa (Mobeto) alikuwa ni rafiki mzuri sana kwangu ingawa siku hizi kuna watu kwenye mitandao wanamuaribu na amekuwa tofauti na mwanzo,” alisema Esma akimzungumzia Mobeto ambaye amezaa na Diamond mtoto mmoja wa kiume aitwaye Dyllan.

Stori: Shamuma Awadhi, Dar

Loading...

Toa comment