Ester Kiama Adaiwa Kuficha Ujauzito

WAKATI wengine wakiona kubeba ujauzito ni ufahari, kwa mwigizaji wa filamu Bongo, Ester Kiama ni tofauti kwani anadaiwa kuuficha na hatoki ndani kwa sasa.

 

Chanzo makini kiliiambia Shusha Pumzi kuwa, Ester kwa sasa ana ujauzito mkubwa, lakini hapendi kutoka nje kwani anahofia kuonekana kwa watu na kuwa wanaweza kumfanyia ndumba.

Shusha Pumzi ilimtafuta Ester na kumuuliza kulikoni kuficha ujauzito ambapo alisema hapendi kutokatoka kwa sababu anafuata mila za zamani kwani ukiwa katika hali hiyo ukitembea hovyo unaweza kukumbana na husda.

 

“Yaani kwa sasa sihitaji picha za kuonesha tumbo langu kama wanavyofanya wengine wala kuonekana mitaani kwa sababu mimba yangu siyo fasheni, hiki ni kiumbe, kipo ndani ya tumbo, kinahitaji heshima maana wengine wana macho ya husda hivyo ni vizuri tukaishi kama wazee wa zamani maana hawakuwa na Snapchat wala Instagram,” alisema Ester.


Loading...

Toa comment