Stori: Gladness Mallya | RISASI JUMATANO | DAR ES SALAAM
STAA wa filamu za Kibongo, Ester Kiama wiki iliyopita aliponea chupuchupu kula kipigo kutoka kwa raia wenye hasira baada ya kutaka kumgonga mtembea kwa miguu.
Chanzo katika eneo la tukio, Kinondoni-Biafra kilisema Ester akiendesha kwa mwendokasi, almanusura amgonge mtu aliyekuwa anavuka barabara kabla ya kufunga breki ghafl a na mara raia wakamzunguka wakiwemo vijana wa kihuni waliotaka kumpa kipigo.
“Yaani ni Mungu tu, maana nilikuwa naendesha sijui hili wala lile mara nikajikuta nikimkosakosa mtembea kwa miguu, akachukua mawe na kutaka kuvunja kioo, huku nikizingirwa na watu kibao wakiwemo vijana wa kihuni wakitaka kunishambulia ila nashukuru Mungu walitokea watu wanaonifahamu wakaniokoa,” alithibitisha Ester baada ya kuulizwa.