Ester Kiama Aogopa Wanga

Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Ester Kiama.

 

WAKATI mwaka 2018 ukielekea ukingoni, mwigizaji wa sinema za Kibongo, Ester Kiama ameogopa kutaja malengo yake ya mwaka ujao wa 2019 kwa kuhofia wanga watamkwamisha.

 

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Ester alisema mwaka ujao anatarajia kufanya kitu kikubwa, lakini hawezi kukitaja kwa kuwa wanga watampiga juju na kushindwa kufikia malengo yake.

 

“Nimejifunza kwamba kwa mwaka huo unaoanza ni vyema nikafanya vitu kimyakimya hadi vikamilike maana nikianza kutangaza, wanga wasiopenda maendeleo yangu, wataya-katisha fasta na kujikuta nashindwa kusonga mbele,” alisema Ester aliyeigiza sinema nyingi ikiwemo Muhanga.

Na Imelda Mtema, Dar

Loading...

Toa comment