The House of Favourite Newspapers

ESTER KIAMA APONDA PENZI LA MAPEDESHEE

Ester Kiama

 MSANII wa filamu za Kibongo, Ester Kiama amewaponda mapedeshee wa mjini waliokuwa wakimwaga pesa kwa wanawake kuwa kwa sasa wame­kuwa zilipendwa kwani mastaa wengi wanaangalia mapenzi na sio pesa zao tena. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Ester alisema mastaa wengi wameg­undua mapenzi ya kweli hayapo kwa mapedeshee ambao walikuwa wana­watumia tu kupitia hela zao.

“Unajua zamani mapedeshee walikuwa wakitumia mifuko yao kuwarubuni mastaa mbalimbali lakini sasa mambo yamebadilika, wengi wa wasichana sasa hawatazami pesa bali mapenzi ya kweli na ndio maana ukichunguza utaona mastaa wanatoka na wanaume wa kawaida sana ambapo wakati mwingine si rahisi kuamini,” alisema Este

Comments are closed.