The House of Favourite Newspapers

ESTER KIAMA ARUDI KIJIJINI KULIMA

Image result for Ester Kiama
Ester Kiama

MWIGIZAJI wa filamu za Ki­bongo, Ester Kiama ameamua kurudi kijijini kwao, Dumila mkoani Morogoro kuan­galia kama anaweza akajishughuli­sha zaidi na kilimo kuliko kupoteza muda mwingi akiwa mjini.  Kiama aliliambia Ijumaa Wikien­da kuwa, anadhani anapoteza muda mwingi mjini, wakati an­geweza kurudi kijijini na akatafuta namna nyingine ya kupambana na maisha.

Alisema kuna vitu vingi amejaribu kufanya ili tu kwenda na maisha yali­yopo hivi sasa, lakini anaona inakuwa vigumu kukamilisha ndoto nyingi alizo­kuwa nazo kwa sasa hivyo bora ageukie kilimo.

“Kipindi tulichonacho sasa hivi si cha kuchagua nini cha kufanya, ni vyema kujiki­ta kwenye kazi yoyote ambayo unajua inaweza kuku­ingizia kipato kizuri na kuweza kujimudu kimai­sha, maana maisha ya sasa ni magumu mno, yaani hamna kuchagua cha kufanya,” alisema Kiama

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.