The House of Favourite Newspapers

Ester Kiama avamiwa, apewa kichapo ajeruhiwa!

0

WATSAP COVER 1868Hamida Hassan na Imelda Mtema
Staa wa Filamu za Kibongo, Ester Kiama juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vibaka na kuchezea kichapo kisha kuibiwa pesa na simu mbili.

esterqSosi aliye karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, siku ya tukio Ester alitoka viwanja na wenzake, walipofika Kijitonyama jijini Dar yeye akiwa anaendesha gari, aliwashusha wenzake lakini wakati anarudi kwenye gari ili aondoke, wakatokea vijana wawili na pikipiki wakamfanyizia.

Ijumaa lilipopata taarifa hizo lilitinga nyumbani kwa Ester na kumkuta akiwa hoi sambamba na majeraha, alipotakiwa kueleza kilichompata alikiri kufanyiwa unyama huo ambapo alisema anajuta kutembea usiku bila kuwa na mwanaume.

Leave A Reply