Ester Kiama ‘kula bethidei’ Mikumi

kiama (2)Hamida Hassan

MWANADADA anayekuja kwa kasi katika filamu Bongo, Ester Kiama leo atafanya sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa katika Mbuga ya Wanyama ya Mikumi, hafla inayodaiwa kuandaliwa kifahari na tajiri wa madini mwenye makazi yake mkoani Mwanza.

Sosi aliye karibu na staa huyo, ambaye sasa ana umri wa miaka 28, aliliambia  Risasi Mchanganyiko kuwa Ester anayedaiwa pia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dude, kwa sasa anatoka na kigogo huyo wa madini.

Akizungumzia suala hilo, Ester alikiri pati hiyo itafanyika Mikumi, lakini kuhusu kuandaliwa na mtu wake huyo, anayedaiwa kumfuata jijini Mwanza, alisema hayuko tayari kuzungumzia mambo hayo kwani kuna watu wenye nia ya kuharibiana maisha kwa faida zao.


Loading...

Toa comment