The House of Favourite Newspapers

Maabara ya Kisasa Yazinduliwa Mashariki ya Kati na Shirika la Ndege la Etihad

Etihad

SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia Kitengo chake cha Uhandisi (Etihad Airways Engineering) kwa kushirikiana na Lental Textiles AG wamezindua maabara ya kipekee ya kwanza Mashariki ya Kati kwa ajili ya wateja wa kanda hiyo walio sekta ya anga na waendeshaji mashirika ya uzalishaji na ubunifu.

Maabara hiyo ambayo ipo ndani ya kituo cha uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abu Dhabi itakuwa inatoa huduma mbalimbali   ikiwemo vipimo vya kuwaka kwa moto, joto, moshi n.k.

Aidha, maabara hiyo itaenda sambamba na hadhi ya ubora wa Kimataifa ISO 17025  na vipimo vyote vitafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Anga za imataifa FAR/CS25.853.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad Jeff Wilkinson alisema, “Tunatoa huduma zilizotukuka kwenye matengenezo ya ndege na ufumbuzi wa kiuhandisi katika soko la anga duniani na kwa ajili ya aina zote za ndege za kibiashara.

“Kupitia ushirikiano wetu huu na Lantal, itakuwa rahisi sasa na haraka kwa kwa wateja wa sekta ya anga katika Ukanda kupata huduma bora za vipimo katika kituo chetu cha Abu Dhabi,” alisema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Lantal, Dkt. Urs Rickenbacher alisema, “Maabara yetu ya Lantal kwa ajili ya vipimo nchini Uswisi inajulikana vema kwa huduma zake bora na haraka.  Kwa sasa tunalo soko kubwa barani Ulaya na sasa maabara yetu hapa Abu Dhabi tukishirikiana na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad (Etihad Aiways Engineering) litatuwezesha kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wateja wetu wa Mashariki ya Kati,”.

etihad (1)

Katika hafla ya uzinduzi wa maabara ya Lantal katika Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad mjini Abu Dhabi. Wanaoshuhudia tukio hilo (toka kushoto kwenda kulia), Peter Baumgartner, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Dkt. Urs Rickenbacher, Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Lantal, Bernhard Randerath ambaye ni Makamu wa Rais, Upangaji, Uhandisi na Ubunifu katika Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad, Heiko Nüssel,  Mdau mwenza, mtendaji makamu wa rais, udhibiti na uhakiki, Lantal; Shevantha Weerasekera,  Mkuu wa Uhandisi, Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad, Jeff Wilkinson na Balozi mdogo wa Uswisi, Jürg Metz

NOTISI KWA WAHARIRI

Kuhusu Lantal Textiles:

Lantal ni kampuni inayoongoza kwa ubunifu, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma za ndege, treni, mabasi na vifaa muhimu vya ndani ya ndege. Kampuni hiyo pia huwa inatoa ushauri kwa wateja wao kwa ajili ya kujenga umoja na kutimiza  malengo yenye tija kubwa hususani kwa abiria. Kwa taarifa zaidi tembelea: lantal.com

Kuhusu Etihad Airways Engineering:

Etihad Airways Engineering ni karakana kubwa zaidi kwa ajili ya kutengeneza na kuzifanyia maboresho mbalimbali ndege zilizopo Mashariki ya Kati.

Ikiwa ni sehemu ya miliki za Etihad Aviation Group, Kitengo hiki hutoa huduma mbalimbali zinazohusiana na ndege za kibiashara ambapo kipo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abu Dhabi.

Kuhusu Etihad Aviation Group:

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad (EAG) linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika saba mengine ambayo; Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi chini ya  Etihad.

Shirika la Etihad lenye makao makuu yake Abu Dhab limejiwekea malengo ya kuhudumia abiria  na usafirishaji mizigo maeneo zaidi ya  110 na kutoa huduma bora ya usafirishaji mizigo Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boing 120, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa;  ikiwamo  71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s na 10 Airbus A380s.

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Kwa mawasiliano zaidi

Elie Dib, Etihad Airways Engineering

Work: +9712 511 2422 / EDib@etihad

Comments are closed.