The House of Favourite Newspapers

Etihad Lazindua Safari za Ndege kati ya Dar na Abu Dhabi

UAE Ambassador to Tanzania Abdullah Ibrahim Al Suwaidi (R) welcomes Etihad Airways’ Senior Vice President - Global Sales, Daniel Barranger (L) upon the arrival of Etihad Airways’ inaugural flight to Tanzania at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam on Tuesday December 1, 2015. PHOTO | FARAJA JUBE

Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger akisalimiana na Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika hilo uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijiji Dar es salaam. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania  kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi.

CROP 2

Wageni na maafisa wa shirika la ndege la Etihad wakishiriki katika hafla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Shirika hilo hapa nchini. Pichani nia Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi Wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania (Katikati), Daniel Barranger, Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad (wa nne kulia), Dr. Shaaban Mwinjaka Katibu Mkuu, Wizara Ya Uchukuzi (wa pili kulia), Mh. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Kwa Umoja wa falme za Kiarabu (wa nne kushoto),  Mhandisi Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege-Tanzania (wa kwanza kushoto),  Ahmed Al Shehhi-Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ndege la Etihad Tanzania (wa kwanza kulia).

CROP 1

Ndege iliyozinduliwa na Shirika la Ndege la Etihad ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kupokelewa na magari ya zimamoto kwa kumwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege za shirika la ndege la Etihad lenye makao mkuu Abudhabi. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.

CROP 2c

Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger (katikati) akifurahia kikundi cha ngoma mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika hilo la ndege hapa nchini. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo sasa wateja mbalimbali watakua na fursa ya kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.

Etihad Airways’ Senior Vice President - Global Sales, Daniel Barranger (L) speaks at a press conference as the UAE Ambassador to Tanzania Abdullah Ibrahim Al Suwaidi (R) looks on after the arrival of Etihad Airways’ inaugural flight to Tanzania at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam on Tuesday December 1, 2015. PHOTO | FARAJA JUBE

Makamu wa Rais- Mauzo Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger (kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa shirika la ndege la Etihad ambao ulifanyika siku ya jana jijini Dar es salaam.Pamoja nae ni Mh. Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi.

Dr Shaaban Mwinjaka, Permanent Secretary, Tanzanian Ministry of Transport speaks at a press conference as the UAE Ambassador to Tanzania Abdullah Ibrahim Al Suwaidi (R) and Etihad Airways’ Senior Vice President - Global Sales, Daniel Barranger (C) look on after the arrival of Etihad Airways’ inaugural flight to Tanzania at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam on Tuesday December 1, 2015. PHOTO | FARAJA JUBE

Katibu Mkuu, Wizara Ya Uchukuzi Dr. Shaaban Mwinjaka akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika la ndege la Etihad uliofanyika katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo sasa wateja watakua na fursa ya kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku (Katikati) ni Makamu wa Rais- Mauzo Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger na (wa kwanza kulia) ni Mh. Balozi wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi.

CROP 8

Wahudumu wa Shirika la ndege la Etihad kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi rasmi wa shirika hilo uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi.

SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za Kiarabu, leo hii imeendelea kuimarisha uwepo wake Afrika Mashariki kwa kuzindua huduma zake mpya za safari za ndege baina ya Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi nchini Tanzania na Abu Dhabi, mji mkuu wa Falme za kiarabu (UAE).

Mara baada ya ndege inayozinduliwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, ililakiwa na mizinga ya maji kama ishara ya heshima kubwa na abiria walioshuka wakikaribishwa kwa burudani ya ngoma za kitamaduni za Tanzania.

Shughuli ya kukata utepe ilifuatia ambayo katika kuweka kumbukumbu ya tukio hilo la kufana ambapo lilifanikishwa na

–        Dr Shaaban Mwinjaka, Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi

–        Dr Adelhelm James Meru, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Maliasili

–        H.E. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Nchi za Falme za kiarabu

–        H.E. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi wa Nchi za Falme za kiarabu Tanzania

–        Daniel Barranger, Makamu wa Rais wa Mauzo ya kimataifa wa shirika la ndege la Etihad

–        Mhandisi:Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege

Dar es Salaam imekuwa ni kituo cha tatu kwa shirika la ndege la Etihad Afrika Mashariki, baada ya Nairobi na Entebbe,na ya tisa barani Afrika.

Huduma hii mpya ikiwa inaendeshwa na ndege aina ya Airbus A320 yenye madaraja mawili, siti 16 daraja la “Business” na siti 120 daraja la “Economy” ikiwa imelenga wafanya biashara na wanaosafiri kwa starehe moja kwa moja kila siku baina ya Dar es salaam na Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji mrahisi kwenda nchi nyingine ukanda wa GCC, Ulaya, India, Asia kaskazini, Asia ya Kusini na Australia.

Bw. Barranger, alisema “uzinduzi huu wa safari za shirika la ndege la Etihad kuja Dar es Salaam zimewiana na mkakati wetu wa kulenga masoko yanayo endelea kukua kwa kasi”.

“Dar es Salaam ni mji ambao umekuwa kivutio sana kwa watalii wanaotaka kufahamu tamaduni na historia ya Tanzania, pia ni mlango wa vivutio vya kitalii vingi vya kitaifa na kimataifa ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama kama Serengeti na kisiwa cha Zanzibar.

“Nchi Falme za kiarabu ni mdau mkubwa wa kibiashara na Tanzania, huduma hii mpya itaongeza nguvu ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili. Ratiba za safari za ndege zitawapa wageni urahisi wa kupata ndege za kuunganisha safari kwenda nchi nyingine, ikiwa inahudumia safari nyingi sana baina ya Tanzania na nchi nyingi katika mtandao wetu wa kimataifa kama Ahmedabad na Mumbai nchini India au Beijing na Shanghai nchini China.”

“Pamoja na kutoa huduma ya moja kwa moja kwa watalii na wafanya biashara baina ya nchi hizi mbili, safari hizi pia zimeendelea kuimarisha uwepo wetu Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla” aliongezea.

Shirika la ndege la Etihad limekuwa likiongeza uwepo wake barani Afrika tokea walipozindua safari zake za kwanza barani Afrika, huko Cairo November 2004. Baada ya hapo zikafuatia Casablanca, Entebbe, Johannesburg, Khartoum, Lagos, Nairobi, (15 January 2015) na Mahe huko visiwa vya shelisheli na mipango ya uzinduzi katika mji wa Rabat, Morocco katikati ya mwezi Januari 2016.

Flight No. Kutoka Kuondoka Kwenda Kufika Idadi Ndege
EY681 Abu Dhabi (AUH) 8:20 Dar es Salaam (DAR) 13:00 Kila Siku A320
EY682 Dar es Salaam (DAR) 13:50 Abu Dhabi (AUH) 20:15 Kila Siku A320

Ratiba za shirika la ndege la Etihad, Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 December 2015:

Zingatia: Muda wa kuondoka ni majira ya Dar es Salaam.

Comments are closed.