The House of Favourite Newspapers

Etihad Yaandaa Mafunzo Ya Kuhamasisha Masomo Ya Sayansi

0

Shirika la Anga la Etihad (EAG) limeandaa kozi maalumu kwa wahandisi na marubani inayofahamika kama ‘Think Science 2017’ katika taaluma ya anga ikiwa ni sehemu ya juhudi za Taifa la Abu Dhabi kuwahamasisha vijana kwenye masomo ya sayansi na teknolojia.

Tukio la uzinduzi wa kozi hiyo lilifanyika katika Ukumbi wa Dubai World Trade Centre na liliandaliwa naTaasisi ya Emirates Foundation ikiwa ni miongoni mwa maonyesho makubwa katika ukanda huo.

Mgeni rasmi katika maonyesho hayo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Emirates Foundation, alizundua maonyesho hayo kisha kutembelea ofisi za Shirika la Anga la Etihad.

Wageni watakaotembelea ofisi za shirika hilo watafahamu mambo mbalimbali ya uendeshaji yanavyofanyika na watajifunza jinsi ya ndege zinavyorushwa.

Marubani na watumishi wa ndege watajibu maswali mbalimbali kutoka kwa watu wanaopenda kufahamu kuhusu masuala ya anga.

Wawakilishi wa Kitengo cha Etihad Airways Engineering watakuwepo, wataonyesha injini ya kisasa ya ndege ya jet, vilevile watatoa ufafanuzi masuala yanayohusiana na ndege ya 120-plus.

Pia, kutakuwa na picha za video zinazoonyesha shughuli mbalimbali za Shirika hilo jinsi linavyojihusisha na maendeleo katika ugunduzi wa mafuta ya ndege ambayo ndiyo wa kwanza katika kuyatumia kupitia mradi wake wa Sustainable Bioenergy Reseach Consortium.

Kapteni Salah Al Frajalla wa Shirika la Ndege la Etihad, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Masuala ya Usalama na Shirika la Taifa la Kuendeleza Maruba ni alisema, “Hii ni chachu ya maendeleo kwa Nchi ya Falme za Kiarbu kutoka na na kuwahamasisha vijana kujiingiza kwenye taaluma ya urubani ambapo watakuwa na ujuzi huu.

Tunatumaini kwamba kuanzishwa Think Science 2017 itawavutia na kuwatia moyo vijana wengi kuanza kujadili masuala yanayohusiana na sayansi na teknolojia.

Piakuhimiza vijana wengine wa Nchi za Falme za Kiarabu kupenda taaluma hii hata kutamani kujiunga na Shirika la Anga la Etihad.

Pia, katika kuwafanya wageni wavutiwe na kuelewa zaidi kuhusu masuala mbalimbali ya Shirika la Anga la Etihad, wageni watapata fursa ya kushindana ili kujishindia safari moja maalumu ambapo wataweza kutembelea na kufahamu shughuli za Shirika la Anga la Etihad linaloongoza kwenye sekta ya anga nchini Abu Dhabi.

Zawadi zitatolewa kwa vijana watakao onyesha ubunifu kwenye masula ya uhandishi wakati wa mashindano hayo.

Maonyesho ya Think Science yalizinduliwa mwaka 2012 yakiwalenga kundi la miaka 15-35 na kuwapeleka maelfu ya wageni kila mwaka . Lengo la serikali ni kuhamasisha ushiriki anao baina ya wanasayansi nawadau wa sekta ya sayansi na teknolojia.

Leave A Reply