The House of Favourite Newspapers

EU Kuipa Tanzania Bilioni 70 Kupambana na COVID19

0

Umoja wa Ulaya (EU) umesema uko tayari kutoa Euro 27 milioni (TZS 70 bilioni) kwa serikali ya Tanzania kwa lengo la kusaidia mipango ya kukabiliana na janga la virusi vya corona pamoja na madhara yake kiuchumi.

 

Charled Michel, Rais wa Baraza la EU amesema hayo akipokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Jestas Nyamanga ambaye pia ni mwakilisha wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya.

 

Nyamanga amehimiza umuhimu wa EU kuondoa marufuku za safari kwa nchi ambazo maambukizi ya COVID19 yamedhibitiwa ikiwemo Tanzania ili kuwezesha sekta mbalimbali kukua ikiwemo utalii.

 

Aidha, balozi huyo ameishukuru EU kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwaletea Watanzania maendeleo kupitia programu mbalimbali.

Leave A Reply