Everjobs Kurahisisha Ajira Nchini
Kutoka kushoto ni Managing Director wa Ever Jobs, Eric Laver,Ofisa Mkuu wa masoko, Lukas Masson pamoja na Country Manager, Florens Roell.
Ofisa Mkuu wa Masoko, Lukas Masson (mbele) akitoa ufafanuzi kwenye uzinduzi huo.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa ajira na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Lukas Masson (mbele) akitoa maelekezo ya jinsi ya kutafuta ajira kwa kutumia teknolojia hiyo mpya.
Mmoja wa wadau akiuliza swali kwa viongozi hao juu ya huduma hiyo ya kiteknolojia.
Maswali yakiendelea kuulizwa kwa viongozi hao juu ya huduma yao mpya.
Managing Director, Eric Laver wa Ever Jobs akielezea kwa kutumia ‘skrini’ namna ya kutumia mfumo huo mpya wa utafutaji ajira.
Hafla hiyo ikiendela.
Eric (kushoto) akifafanua jambo.
Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Ever Jobs (kulia),Benson Mgideon.
TANZANIA tayari kuanza kunufaika na huduma ya tovuti Everjobs inayolenga kurahisisha utafutaji wa kazi na mchakato wa kuajiri kwa kuwaunganisha wanaotafuta kazi na waajiri kwa haraka.
Akizungumza kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Eric Laver alisema kuwa tovuti hiyo ni kiungo muhimu katika soko la ajira nchini kwa kuwa imelenga kutoa mwongozo rahisi na unaoeleweka haraka kama vile uwekaji wa CV ya mwomba ajira na kuona nafasi za kazi zilizowazi kutoka kwenye kampuni mbalimbali zinazotoa ajira.
Mbali na hayo tovuti hiyo imerahisisha mchujo wa utafutaji wa waajiriwa wanaokidhi viwango vya kampuni husika kutokana na matakwa ya waajiri.
Eric Laver alisema kuwa tovuti hiyo inatoa fursa kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kujiingiza katika soko la ajira kutokana na taaluma zao huku nafasi za kuajiriwa katika nchi jirani kama vile; Cameroon, Ivory Coast, Senegal, Uganda na Ethiopia zikipatikana kwa urahisi.
Akizungumzia mafanikio ya tovuti hiyo wiki chache tangu kuanzishwa kwake, mkurugenzi huyo alisema kuwa ina waajiri wakubwa zaidi ya mia moja huku ikiwa imepata waomba ajira zaidi ya 30,000 idadi ambayo inaongezeka kila kukicha.
Kwa maswali yoyote na ufafanuzi wa jinsi ya kutumia waombaji wanaweza kuwasiliana nao kupitia everjobs.co.tz na kwa kutumia mtandao wa Facebook, Linkedin, Tweeter na Instagram.
Picha/Denis Mtima na Chande Abdallah/GPL