The House of Favourite Newspapers

Everton Yakatwa Pointi 10 Kwa Kukiuka Kanuni Za Fedha

0

Everton wamekatwa pointi 10 kwa kukiuka kanuni za kifedha (Financial Fair Play) za ligi Kuu Uingereza katika kipindi kilichoishia msimu wa 2021/22.

Alama hizo zinakuwa ni alama kubwa zaidi kukatwa kwa timu katika historia ya Ligi Kuu ya England na yanaitumbukiza timu ya Sean Dyche kwenye eneo la kushuka daraja.

Everton walikuwa, kabla ya kupoteza pointi zao, wakiwa nafasi ya 14 kwenye jedwali la ligi, pointi nane juu ya timu tatu za mkiani. Ni klabu mbili pekee ambazo hapo awali ziliwahi kupokwa pointi katika historia ya Ligi Kuu – Middlesbrough, ambao walikatwa tatu kwa kushindwa kutimiza mechi dhidi ya Blackburn msimu wa 1996/97 na Portsmouth, ambao walipokonywa pointi tisa mnamo Machi 2010.

A-Z HUKUMU YA SABAYA,MAJAJI WASHANGAZWA NA USHAHIDI WA SERIKALI WASEMA HAKUSTAHILI KUFUNGWA MIAKA 30

Leave A Reply