EWURA Yaandaa mfumo uitwao EWURA e-LUC kufuatilia utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeandaa mfumo uitwao EWURA e-LUC, ili kufuatilia utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira katika kuwahudumia wateja wake. Mfumo huu unalenga kupata taarifa za kiwango ambacho wateja wanahudumiwa na kufahamishwa haki zao za msingi kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Mamlaka ya Maji.
Kwa kuanzia, mfumo huu (EWURA e-LUC) utatumika kupata mrejesho kutoka kwa wateja wa DAWASA
Tafadhali, EWURA inakuomba ujaze fomu ya EWURA e-LUC kwa kubonyeza link ifuatayo: https://forms.gle/94vdRu87yQ1rWwKs6.
Kwa maelezo au ufafanuzi zaidi unaweza kupiga simu 0800110030 au kutuma barua pepe kupitia [email protected]
Asante kwa kushiriki zoezi hili.
Limetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
EWURA