Ewura Yazitaka Mamlaka za Maji Kusoma Mita Mwenyewe Akiwepo

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imezitaka mamlaka zote za maji nchini kuhakikisha zoezi la usomaji wa mita linafanyika pindi mwenye mita anapokuwepo wakati wa zoezi hilo ili kuepusha mkanganyiko unaoweza kujitokeza.
Akizungumza wakati wa akitoa mafunzo ya uthibiti wa huduma za nishati na maji, kwa Chama Cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka EWURA Titus Kaguo amesema ukataji wa maji katika siku za mwisho wa wiki huku akiwataka Watanzania kusoma mikataba ya huduma za mamlaka za maji ili kujua haki na wajibu wa msingi katika mikataba hiyo.

Amesema mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ilishatoa miongozo huko nyuma ambayo inataka usomaji wa mita za maji uwe anasoma mita wakati mtu mwenye mita kwa maana ya mmiliki akiwepo.
Sio unasoma mmiliki wa mita hayupo ,anatakiwa mmiliki wa mita awepo katika eneo la mita;
“Kwanini EWURA iliagiza hivyo kulikuwa na malalamiko ya kubambikiziwa bili kwa maana ya kwamba watumishi wa mamlaka mbalimbali wanafika mahala halafu wanakuletea hii ndio bili yako. Sasa tukatoa agizo mita zinaposomwa kwanza mwenye mita awepo.

“Na baada ya kusoma wote wakiwemo utatumwa ujumbe kwenye simu na tunaamini Watanzania wanaupata ule ujumbe ambao unaweza kuwa unakuambia mita tuliyoisoma inasema Kiasi hiki na unatolewa muda wa siku mbili au tatu kwa ajili ya kujadiliana kwamba hii bili iliyoletwa ni halali au si halali.
“Ukishakaa siku tatu bila majibu wanakuletea bili halısı ya kulipa ,kwahiyo baada ya kufanya hivyo tunaona malalamiko yanapungua. Lakini kingine ambacho tuliagiza ni marufuku kwa mamlaka ya maji kukata maji siku za mapumziko kwasababu kuu inakuwa kama unyanyasaji.
“Kama mtu anakuwa na makosa mkatie siku ambayo atakuja ofisini kutatua kosa ili huduma irudi, kwa hiyo hii ya kusema mtu anakata siku ya Ijumaa saa 12 jioni hiyo hairuhusiwi kitaratibu na wala hairuhusiwi kiudhibiti na mamlaka inayofanya hivyo itakuwa inakosea na haitakiwi kufanya hivyo sababu inaweza kuchukuliwa sheria ili kuwajibika kwa kile wanachokifanya, ”amesema Kaguo.
Naye Mhandisi Mwandamizi wa Umeme wa Mamlaka hiyo Mwanamkuu Kanizio, amesema Ewura itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuhamasisha matumizi ya mafundi wenye leseni lakini pia imeunganisha mfumo wa utoaji wa leseni na mfumo wa uunganishaji wa umeme ili kurahisisha uunganishaji wa umeme kwa wananchi.
Kwa upande wake, Seleman Msuya ambaye ni Katibu Mkuu wa JOWUTA amewataka wanahabari kuwa mabalozi wa kueleza taarifa sahihi zinazotolewa na Ewura ili kuwezesha wananchi kupata huduma hizo kwa ufanisi.